Yanga yasaka rekodi nyingine ya 'unbeaten' ligi kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Feb 2026
Yanga yasaka rekodi nyingine ya 'unbeaten' ligi kuu

Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC hapo jana ulikuwa na maana kubwa kwa Wananchi.

Ukiacha thamani ya alama hizo tatu walizopata ugenini, ushindi huo unawaweka karibu na rekodi nyingine ya kutopoteza mchezo kwa muda mrefu kwenye ligi kuu.

Ni hivi; mara ya mwisho kwa Yanga kupoteza mchezo kwenye ligi kuu ya NBC ni Novemba 07 2024 ikichapwa mabao 3-1 na Tabora United katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex.

Tangu wakati huo, Yanga haijapoteza tena mechi ya ligi kuu kwa takribani miezi 15 wakicheza mechi 29.

Kama Wananchi hawatapoteza mchezo unaofuata dhidi ya JKT Tanzania basi watafikisha mechi 30 bila ya kupoteza mchezo ambapo ni sawa na kucheza msimu mzima.

Msimu huu Yanga tayari imecheza mechi 9, ikishinda nane na kutoka sare mchezo mmoja. Ni msimu mwingine kwa Wananchi kuweka rekodi ya kibabe.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’