Kiungo mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize yuko Afrika Kusini akiendelea n matibabu kutokana na changamoto ya majeraha inayomsumbua.
Nyota wa zamani wa Yanga Skudu Makudubela alipata nafasi ya kumjulia hali Mzize ambaye msimu huu amekumbwa na changamoto kubwa ya majeraha.
Skudu kwa sasa anaitumikia klabu ya Siwelele Fc inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini.
Licha ya kuondoka Yanga misimu miwili iliyopita, Skudu bado ameendelea kuwa karibu na Wananchi akiweka wazi kuwa yeye atabaki kuwa shabiki wa Yanga.

ADVERTISE HERE