Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua anashiriki kikamilifu maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Jumapili, March 1 uwanja wa New Amaan Complex.
Pacome alikuwa nje ya uwanja kwa takribani siku 10 akiuguza majeraha ya bega aliyopata kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie.
Pacome alionekana kujumuika na wenzake kwenye mazoezi tangu siku ya jana ikiwa ni ishara ya kuwa tayari kuikabili Simba siku ya Jumapili.
Yanga leo imeingia siku ya pili ya maandalizi yake visiwani Zanzibar kuelekea mtanange huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.






ADVERTISE HERE