Baada ya ushindi muhimu wa mabao 3-0 dhidi ya Singida BS hapo jana, kikosi cha Yanga leo kinarejea jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo unaofata.
Jumapili March 08 Yanga inakabiliwa na mchezo wa hatua ya 32 bora kombe la CRDB dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa uwanja wa KMC Complex.
Yanga imeondoka mkoani Singida kuelekea Dodoma ambako itaunganisha na treni ya SGR kurejea Dar es salaam.
Baada ya kumalizana na Polisi Tanzania siku ya Jumapili, Yanga itaondoka Dar kuelekea mkoani Mbeya wanakokabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons March 12 ukitarajiwa kupigwa dimba la Sokoine.
Pichani juu ni Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kiwa pamoja na Wanafunzi wa Kituo cha Sabasaba Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye ulemavu baada ya mchezo Singida Black Stars.
Uongozi wa Yanga ulinunua tiketi kwa ajili ya Wanafunzi hao kushuhudia mtanange uliopigwa uwanja wa Airtel 'Mwigulu Complex'.