Yanga yaibua maswali adhabu waamuzi wa dabi ya Kariakoo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Mar 2026
Yanga yaibua maswali adhabu waamuzi wa dabi ya Kariakoo

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ally Kamwe, ameibua maswali mazito kufuatia maamuzi ya hivi karibuni ya Kamati ya Saa 72 kuhusu mchezo wa Dabi ya Kariakoo.

Kamati ya saa 72 iliwafungia waamuzi 1&2 kwa kushindwa kutafsiri vyema sheria za mpira wa miguu. Kamwe amesema licha ya waamuzi hao kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni moja ya 42:1(1.8) lakini vifungo vyao havifanani.

"Kamati ya saa 72 imetoa hukumu kwa waamuzi wasaidizi 1&2, kwenye mchezo wa Yanga SC dhidi ya Simba SC baada ya kushindwa kutafsiri sheria namba 11 [OFFSIDE]."

"Waamuzi hao wamehukumiwa kwa kanuni moja ya 42:1(1.8) lakini mmoja amefungiwa miezi 6 na mwingine miezi 3. Tunataka tujue ni SAYANSI gani imetumika hapa kuchanganua adhabu hizi kuwa tofauti ikiwa wote wamefanya kosa la kushindwa kutafsiri sheria moja. Je kamati yetu inayo SAYANSI ya kuona kesho kwa kubaini kuwa Prince Dube asingefunga nafasi ya wazi aliyopata?”

"Kwa mujibu wa sheria za FIFA, goli halali ni lile goli pekee ambalo limeruhusiwa na mwamuzi wa kati. Kinyume na hapo hakuna kamati wala sheria au kanuni ambayo inayo mamlaka ya kuhalalisha goli ambalo halikuidhinishwa na mwamuzi wa kati . Kauli ya kwamba Simba wamenyimwa goli HALALI imeleta taharuki kwa UMMA. Tumeiandikia Kamati itueleze imetoa wapi Mamlaka ya Kutangazia Umma kuwa Goli ni Halali?” 

"Kwenye mchezo wa KMC FC dhidi ya Simba SC, Seleman Mwalimu alifunga bao akiwa katika eneo la kuotea. Kamati iliyosema kuna goli halali limefungwa limekataliwa, ilikuwa bubu kusema kuna goli lisilokuwa halali limekubaliwa, aidha hata mwamuzi msaidizi hakufungiwa kama ambavyo waamuzi wasaidizi wamefungiwa kwenye mechi ya Derby,” alisema Kamwe.

Aidha Kamwe alibainisha mechi nyingine ambazo licha ya waamuzi kufanya makosa ya kushindwa kutafsi sheria mpira wa miguu, hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya yao.

β€œMechi nyingi za Yanga SC kukiwa na makosa yanayohusisha sheria namba 11 (Kuotea/Offside), kamati hii imekua makini sana kufanya maamuzi ya kuwafungia waamuzi. Lakini matukio hayo yakiwa yanaiumiza Yanga kamati hii imegeuka kuwa bubu."

"Mfano mchezo wa Yanga dhidi ya JKT mwamuzi Glory Tesha alizuia matukio mawili ya wazi ya Yanga kufunga kwa madai kuwa wachezaji wetu waliotea. Lakini kwa marejeo ya video iliyonekana kuwa Wachezaji hawa hawakuwa kwenye eneo la Kuotea, Mpaka sasa kamati haijachukua maamuzi kwa waamuzi husika”

Kamwe amesema Yanga inasubiri majibu ya masuala yote waliyohoji kutoka kwa bodi ya ligi bodi itakapojibu watarudi kuwajuza mashabiki na wanachama wa Yanga lakini hata wasipojibu pia Yanga itawafahamisha wanachama wao kuwa hawajajibiwa.

Download Xtra 90 App

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
53m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’