Gadiel Michael afunguka ya moyoni

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
2 Aug 2017
Gadiel Michael afunguka ya moyoni
Mlinzi wa pembeni wa Azam FC na timu ya Taifa ya Tanzania, Gadiel Michael amefunguka juu ya sakata la usajili wake Yanga.

Gadiel amekiri kusaini mkataba wa awali wa kuitumikia Yanga na anaruhusiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za FIFA kwa kuwa mkataba wake na Azam umebaki chini ya miezi sita.

Lakini amedai kusikitishwa na uongozi wa Azam ambao unaonyesha kila dalili ya kutaka kumkwamisha asicheze soka hadi mkataba wake utakapomalizika mwezi Disemba.

Gadiel amesema Azam FC imemuondoa kwenye kikosi chao cha msimu huu lakini cha ajabu hawataki kumruhusu aondoke.

"Nimesaini mkataba wa awali Yanga SC baada ya kuafikiana nao dau zuri na pia mkataba wangu hapa umebaki miezi 5 tu" , amesema.

"Cha ajabu Azam wananibania, wananiwekea 'mtima nyongo' hawataki nifanye mazoezi na timu yao hata chumba changu tayari wamempatia mchezaji mwigine.

"Wamenijibu kuwa sipo katika programe ya mwalimu ila hawataki kuniruhusu niondoke, Inauma sana maana nahitaji kujumuika na timu ili kumantain kiwango changu.

"Nitaendelea mazoezi ya gym wakiamua nicheze sawa wasipotaka yote namwachia Mungu, mie nimeshapitia mengi na hakika haya yatapita tu," amefunguka Gadiel.

Uchunguzi tuliofanya tumebaini ni kweli Gadiel hayumo kwenye kikosi cha Azam FC na si miongoni mwa wachezaji waliorodheshwa kwa ajili ya msimu ujao.

Naamini swala lake litamalizwa vyema na viongozi wa pande zote mbili kabla dirisha la usajili halijafungwa Agosti 06. Azam lazima wafahamu mpira wa sasa ni biashara hawana haki ya kumzuia mchezaji kama anataka kuondoka.

Tujifunze kutoka kwa wenzetu Ulaya, si kosa kwa mchezaji kusaini mkataba wa awali na timu nyingine kama mkataba wake uko chini ya miezi sita.

Lakini pia hata kama Azam FC watagoma kumuuza Yanga kwa lengo la kumkomoa wanaweza kujikuta matatizoni kama watasitisha kumpa huduma stahiki kama mchezaji wao hadi pale mkataba wake utakapomalizika.

Katika miezi mitano hiyo Azam wanatakiwa wamlipe Gadiel mishahara na stahiki zake hata kama wamemuondoa kwenye kikosi chao, kinyume chake mchezaji anaweza kuvunja mkataba na kuruhusiwa kujiunga na timu nyingine hata katikati ya ligi.

Emanuel Okwi aliwahi kuvunja mkataba wake na Etoile Du Sahel kwa mazingira kama hayo ya kukiukwa kwa makubaliano na mkataba na FIFA ikamruhusu atafute timu ili alinde kiwango chake.

Naliona hilo likitokea kwa Gadiel kama Azam watakomaa 'kumbania'.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’