Kiungo Mudathir Yahya ameanza kurejea katika ubora wake baada ya kupona majeraha ambayo yalimfanya akose mechi nyingi za mwanzo wa msimu huu.
Katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Singida BS na jana dhidi ya Polisi Tanzania ukiwa mchezo wa kombe la CRDB, Mudathir alionyesha umahiri wake akifunga ba kutoa pasi za mabao.
Katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, Mudathir na Allan Okello walikuwa mwiba eneo la kiungo kila mmoja alihusika katika mabao mawili.
Mudathir alifunga na kutoa pasi ya bao wakati Okello alitoa pasi mbili za mabao huku pia akisababisha beki wa Polisi Tanzania kujifunga kwenye jitihada za kuokoa shuti lake lililokuwa linaelekea kimiani.
Licha ya kuanza taratibu msimu huu, Mudathir amefunga mabao manne katika ligi kuu ya NBC.
ADVERTISE HERE