Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kukamilisha maandalizi yake leo jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea mkoani Tabora kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaopigwa Alhamisi, March 12, 2026.
Mchezo dhidi ya Tanzania Prisons unatarajiwa kupigwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Prisons wakichagua uwanja huo baada ya dimba la Sokoine kufungiwa.
Wapinzani wao Tanzania Prisons wanatarajiwa kuwasili mkoani Tabora leo wakitokea Mbeya.
Yanga inatarajiwa kutumia usafiri wa ndege hadi Tabora na Wananchi kurejea Dar baada ya kukamilisha mchezo huo.
Siku ya Jumapili, March 15 Yanga inakabiliwa na mchezo mwingine wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao umerejeshwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
ADVERTISE HERE