Kikosi cha Yanga tayari kimerejea jijini Dar es salaam baada ya kuondolewa kwenye michuano ya SportPesa Super Cup kwa kulazwa mabao 3-1 na kakamega HomeBoyza jana.
Wakati Yanga ikiwa imerejea, baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi wamebaki nchini Kenya wakiifuatilia Gor Mahia ambayo itacheza na Yanga Julai 19 kwenye mchezo wa tatu wa kombe la Shirikisho.
Gor Mahia kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya JKU 'ilificha' silaha zake kwa kuwatumia wachezaji wachache wa kikosi cha kwanza.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Dylan Kerr alidai kuwa amelazimika kutumia kikosi tofauti kwenye michuano hiyo kwa kuwa timu yake inakabiliwa na mashindano mengi.
Mshindi wa michuano ya SportPesa Super Cup atapata kikombe, pesa taslim Mil 68 na kupata nafasi ya kwenda Uingereza kucheza na Everton.

ADVERTISE HERE