Hii ya Azam Fc imepita, nyingine zinafuata

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Mar 2026
Hii ya Azam Fc imepita, nyingine zinafuata

Jana Yanga ilikuwa uwanja wa Benjamin Mkapa ikimenyana na Azam Fc katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC.

Mchezo huo uliotawaliwa na mbinu za makocha zaidi, ulishuhudia nafasi chache zikitengenezwa huku timu zikigawana vipindi.

Azam Fc walianza kwa kasi wakifanya mashambulizi mengi langoni kwa Yanga kwenye dakika 30 za kwanza lakini ni shambulizi moja tu la hatari ambalo lilimshughulisha mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra dakika za mwanzo.

Kipindi cha pili ni Yanga iliyomiliki mchezo kwa muda mwingi na kutengeneza mashambulizi kadhaa ambayo mengine yaliishia njiani kwa kuokolewa na Azam Fc au makosa ya wachezaji wenyewe.

Kuingia kwa Pacome Zouzoua kwenye kipindi cha pili kuliiongezea Yanga makali hasa kwenye eneo la mwisho, waliongeza presha kwenye lango la Azam Fc, pengine wananchi walistahili kupata mkwaju wa penati dakika za lala salama.

Yanga ilizihitaji alama zote tatu lakini hata alama moja waliyopata ina thamani kubwa hasa ikizingatiwa wamecheza dhidi ya timu ambayo pia inataka ubingwa.

Azam Fc msimu huu ni timu ngumu kufungika, hawajapoteza mchezo kama ilivyo kwa Yanga. Huo ulikuwa mchezo wa 18 mfululizo wanacheza kwenye ligi bila ya kupoteza huku Yanga wakifikisha mechi ya 34.

Katika mchezo huo Yanga haikuonekana kufunguka sana, mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves aliamua timu yake icheze kwa tahadhari na wakati mwingine kushambulia kwa kushitukiza wakitambua hatari waliyonayo Azam Fc hasa kwenye mashambulizi ya kujibu.

Lakini pia ikumbukwe huo ni mchezo wa tano Yanga imecheza katika kipindi cha siku 15. Ni wastani wa kucheza mechi kila baada ya siku tatu. Zipo nyakati uliona uchovu walionao wachezaji, hali hii pia inawezekana iliathiri ufanisi wao na kufanya maamuzi.

Yanga na Azam Fc zote zimekabiliwa na ratiba ya mechi mfululizo, kwa makocha alama matokeo hayo yalikuwa fair kwa timu zote.

Hakuna muda wa kulalamika kwani katika kipindi cha siku tano, Yanga inakabiliwa na mechi nyingine mbili za ligi kuu. Jumatano wanacheza dhidi ya TRA United (Arusha) na Jumamosi wanacheza dhidi ya Mtbwa Sugar(Dodoma).

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’