Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema kikosi chake kimejiandaa kukabiliana na mechi ngumu dhidi ya TRA United itakayopigwa kesho Jumatano, March 18 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Goncalves alisema anatambua ugumu wa mchezo huo hasa kwa kuzingatia ubora wa TRA United ambayo imekuwa ikiimarika siku hadi siku.
Pedro amesema vijana wake wamecheza mechi ngumu siku mbili zilizopita dhidi ya Azam Fc na kesho wanakwenda kucheza mechi nyingine ngumu dhidi ya TRA United.
"Kesho itakuwa mechi yetu ya mwisho kukamilisha mzunguuko wa kwanza wa ligi. Tumejiandaa kucheza mechi ngumu dhidi ya TRA United, miongoni mwa timu zilizoimarika sana wakicheza soka la ushindani."
"Tunajua haitakuwa rahisi, tumetoka kucheza mengi ngumu dhidi ya Azam Fc siku mbili zilizopita, wenzetu wamepata takribani wiki nzima ya kujiandaa na mchezo huu baada ya mechi yao iliyopita kutofanyika."
"Pamoja na changamoto zinazotukabili nisema tuko tayari, tunajiamini, tunakwenda kuwakabili TRA United tukiwa na morali kubwa," alisema Goncalves