Bandika bandua inaendelea ambapo baada ya mchezo dhidi ya TRA United uliopigwa mkoani Arusha jana na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana, kikosi cha Yanga kimeondoka Arusha kuelekea Dodoma.
Keshokutwa Jumamosi, March 21 Yanga inakabiliwa na mchezo mwingine wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa uwanja wa Jamhuri. Huo utakuwa mchezo wa saba Yanga inacheza katika kipind cha siku 21.
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema licha ya kukosa alama tatu kwenye mchezo dhidi ya TRA United, timu inakwenda Dodoma ikiwa na dhamira ya kuchukua alama tatu ili kuanza vyema mechi za duru ya pili.







ADVERTISE HERE