Wakati nyota wa Yanga wakipewa mapumziko ya siku chache kabla ya kurejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa April 04 uwanja wa KMC Complex, wachezaji wengine wameelekea kwenye majukumu ya timu za Taifa.
Yanga ina wachezaji wanne kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinachojiandaa na mechi za kirafiki (FIFA Series) zitakazofanyika huko Rwanda kati ya March 26-31 kwa mfumo wa mashindano.
Nyota wa Yanga walioitwa katika kikosi hicho ni Mohamed Hussein, Ibrahim Bacca (majeruhi), Bakari Mwamnyeto na Mudathir Yahya.

Aidha Prince Dube ambaye pia ni majeruhi nae ameripoti timu ya Taifa ya Zimbabwe.
Lassine Kouma amejumuishwa kwenye kikosi cha Chad kitakachocheza dhidi ya Burundi kuwania kufuzu Afcon 2027.
Duke Abuya nae ni sehemu ya kikosi cha Harambee Stars kilichoelekea Rwanda kushiriki FIFA Series