Wakati madaktari wa Yanga wakiendelea kupambana kuwarejesha kikosini wachezaji ambao ni majeruhi, kuna ahueni kidogo kwa Wananchi baada ya baadhi ya wachezaji kuanza mazoezi ya kuimarisha utimamu wa mwili.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa wachezaji Chadrack Boka, Prince Dube na Edmund John wameanza kufanya mazoezi ya Gym.
Nyota hao wanatarajiwa kuanza mazoezi mepesi ya uwanjani karibuni na pengine kuungana na wenzao pale watakaporejea.
Hata hivyo Kamwe amesema wachezaji Ibrahim Bacca na Laurindo Aurelio 'Depu' bado wanaendelea kupata matibabu.
Yanga inatarajiwa kurejea mazoezini mwishoni mwa wiki kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa April 04 kwenye uwanja wa KMC Complex.
ADVERTISE HERE