Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewapongeza mashabiki na wanachama wa timu hiyo kwa kukamilisha zoezi la kuchangisha Tsh Milioni 4 ndani ya saa 24 kwa ajili ya kulipa faini ya mlinda lango Djigui Diarra.
Kamwe amesisitiza mchakato huo ulianzishwa na mashabiki wenyewe kutokana na mapenzi waliyonayo kwa wachezaji wao ambao wanakuwa nao pamoja katika nyakati za furaha na hata katika nyakat ngumu..
Kamwe amesema Wanayanga wamekuwa na utaratibu huo mzuri ambao unawaweka karibu na wachezaji wao.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ameandika ujumbe huu;
"Ndani ya Saa 24, Mashabiki wa Yanga wamechanga kiasi cha Tsh MILIONI 4 kwa ajili ya Golikipa Djigui Diarra
Tunaposema hii ni Timu ya Wananchi hatumaanisha ni katika zile nyakati za Furaha.. Sisi ni wamoja na wenye nguvu pale mmoja wetu anapokuwa kwenye nyakati ngumu
Hili Limepita na ninaamini Diarra amelipokea kwa upendo na deni kubwa moyoni mwake .. In Shaa Allah adhabu yake itakwisha na atarudi akiwa na moroli na Ari ya juu ya kuipambania Klabu yetu kwenye mbio za Ubingwa," aliandika Kamwe
Pamoja na kulipa faini hiyo, Diarra atakosa mechi tatu zinazofuta kwenye ligi na kombe la CRDB