Timu ya Programu ya kuendeleza vipaji ya TDS U17 ndio Mabingwa wa Yanga Soccer School Tournament baada ya kuichapa Fountain Gate Academy kwa Penalti 3-2 baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 kwenye muda wa kawaida.
Mashindano hayo ambayo yalianza jana, yalifanyika maalum kwa lengo la kusaka vipaji ambapo wachezaji 10 watakaochaguliwa baada ya mchujo watanufaika na udhamini wa EMWANI CAFE kujiunga na Yanga Soccer School.
Mchezaji Hassan Kizinga wa TDS U17 alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano huku pia akibeba tuzo ya mfungaji bora.
Tuzo ya Golikipa Bora wa Mashindano imekwenda kwa Shaluni Mohamed Iloko kutoka Fountain Gate Academy.

ADVERTISE HERE