Bacca arejea mazoezini, awaombea Job, Mzize

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Mar 2026
Bacca arejea mazoezini, awaombea Job, Mzize

Beki wa Yanga SC, Ibrahim Bacca, amerejea rasmi kwenye mazoezi ya klabu jana, akiungana na wachezaji wengine waliojifua kwenye KMC Complex, wakijiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Jumamosi, Aprili 4, 2026, kwenye uwanja huo huo.

Bacca, ambaye ni tegemeo kwa Yanga na timu ya Taifa, amesema anajisikia faraja kurejea kikosini. Aidha, amewaombea wachezaji wenzake beki Dickson Job na mshambuliaji Clement Mzize ambao wataendelea kukosa michezo kwa muda mrefu kutokana na majeraha.

Job alipata maumivu katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba SC, uliochezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, na taarifa za awali zinasema huenda akarejea uwanjani kwenye pre-season ya maandalizi kuelekea msimu ujao.

Mshambuliaji Clement Mzize nae msimu huu amekumbwa na majeraha ya kila mara ambayo yamepelekea kufanyiwa upasuaji wa goti mara mbili akitarajiwa kukosekana mpaka mwisho wa msimu

Akizungumza na waandishi kwenye Yanga Media Day, Bacca alisema:

“Mimi kwa upande wangu namshukuru Mungu nimerejea uwanjani ila namiss uwepo wa mwenzetu Job (Dickson), tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu apone haraka hata kwa msimu huu aweze kurejea kwa kuwa kwa Mwenyezi Mungu hakuna kinachoshindikana."

"Sisi tunapambana kwa ajili yake na hata Clement Mzize pia tunamoombea apone haraka kwa kuwa tunaendelea kupambana kuona timu inapata matokeo mazuri uwanjani,” alisema Bacca

Bacca, Chadrack Boka, Edmund John na Prince Dube wameimarika na tayari kurejea kikosini huku Laurindo Aurelio 'Depu' akiendelea kuwa chini ya ungalizi wa daktari.

Mwezi huu March Yanga ilikabiliwa na mfululizo wa mechi hali iliyopelekea majeruhi wengi lakini kipindi cha mapumziko ya kalenda ya FIFA kimewasaidia baadhi ya wachezaji kurejea kikosini kwa wakati.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’