Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua amesema wachezaji wanatambua deni walilonalo kwa mashabiki wao baada ya kuyumba kwenye mechi za ligi kuu karibuni.
Pacome amesema wamerejea mazoezini wakiwa na dhamira moja, kujiimarisha na kuhakikisha wanarejea kwenye ubora wao ili kuwapa furaha mashabiki wao.
"Msimu huu umekuwa mgumu kidogo lakini bado haujaisha. Haya ni mambo ya kawaida kwenye mpira na hata kwenye maisha ya kawaida ziko nyakati za kupita vipindi vigumu"
"Jambo muhimu ni kukubali hali hii na kuongeza bidii uwanja wa mazoezi ili kuhakikisha tunarejea tukiwa imara zaidi."
"Tunapaswa kurudi kwenye kiwango chetu bora ili kuwafurahisha mashabiki wa watu wengini wanaotutegemea."
"Tumerejea mazoezini tukiwa na umakini mkubwa, tutafanya mazoezi kwa bidii ili turejee kwenye ubora wetu na kuwapa furaha mashabiki," alisema.
Kikosi cha Yanga kilirejea mazoezini juzi Jumatatu kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Jumamosi uwanja wa KMC Complex.