Baada ya bandika-bandua ya mwezi March ambayo iliwashuhudia Wananchi wakivuja jasho kwa mechi nyingi ugenini, katika mwezi huu April Yanga itakuwa na ahueni kwa mechi nyingi kucheza nyumbani.
Ratiba mpya iliyoboreshwa na Bodi ya ligi inaonyesha April 04 Yanga itaikaribisha Tanzania Prisons katika mchezo utakaopigwa uwanja wa KMC Complex.
Baada ya mchezo huo, Yanga itaelekea jijini Mwanza kuikabili Pamba Jiji katika mchezo wa ligi utakaopigwa April 08.
April 11 Yanga itarejea KMC Complex kuikabili TMA Stars katika mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la CRDB.
Baada ya mchezo huo Wananchi wataendelea kusalia jijini Dar es salaam ambapo April 16 watacheza na Mbeya City uwanja wa KMC Complex.
Ikumbukwe pia kati ya April 21 na 26 Yanga itakuwa visiwani Zanzibar kushiriki mashindano ya kombe la Muungano.
