Kikosi cha Yanga kimepata wakati nzuri wa kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa kesho Jumamosi, April 04 katika uwanja wa KMC Complex.
Yanga ilirejea mazoezini tangu siku ya Jumatatu ambapo jana timu iliingia rasmi kambini Avic Town kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo huo.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kwa maandalizi waliyofanya, Tanzania Prisons wanapaswa kujiandaa 'kisaikolojia' kwani wanakwenda kukabiliana na Yanga yenye ari mpya na dhamira ya kurejesha makali yao baada ya kuyumba kwenye mechi zilizopita.
Kikosi cha Tanzania Prisons tayari kiko jijini Dar es salaam ambapo leo watapata nafasi ya kukamilisha maandalizi yao katika uwanja wa KMC Complex.
Wananchi wao watakamilisha maandalizi yao Avic Town wakiwa wamerejea rasmi nyumbani baada ya kukamilika kwa maboresho



