Yanga kuifuata Pamba Jiji leo usiku

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2026
Yanga kuifuata Pamba Jiji leo usiku

Leo Wananchi wanaelekea mkoani Mwanza tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji ambao utapigwa Jumatano, April 08 katika uwanja wa CCM Kirumba.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kikosi kitaondoka jijini Dar es salaam leo saa 3 usiku.

Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi ya kikosi chao uwanja wa ndege Mwanza na kuhakikisha siku ya Jumatano wanajitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji.

Kamwe amesema wanatarajia mchezo huo utakuwa mgumu lakini hakuna njia ya mkato ni lazima kushinda kila mechi ili kujihakikishia ubingwa.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ameandika ujumbe huu;

 "Chama Letu Young Africans Sports Club litaondoka Dar Es Salaaam saa 3 Usiku leo kulekea Mwanza, kwa ajili ya game dhidi ya Pamba Jiji itakayopigwa CCM Kirumba April 9.

Tumepata Faida tena ya kuwa na POINTI 3 juu ya kilele pale Juu. Tusirudie makosa tena Wanangu.

Huu Ubingwa Msimu huu unahitaji roho ngumu na mapambano makali ndani na nje ya uwanja. Tuje vitani sasa. Tutoke majumbani, Tuache Uchambuzi kwenye simu zetu, Tutoke mstari wa mbele kuisapoti Timu yetu kila mechi

Mechi ya Pamba Jiji ni ngumu sana Lakini Tukiweka nguvu ya pamoja na wachezaji wetu wakatuona kwa wingi kuanzia mapokezi Leo usiku na wakatuona tena kwa wingi uwanjani siku ya mechi, Sina shaka watatupigania sana tupate pointi 3.

Daima Mbele Nyuma mwiko..

Ni muda wa kuonyesha Ukubwa na Mapenzi yetu kwa chama Letu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’