Ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji jana umeifanya Yanga ifikishe mechi 38 za ligi bila kupoteza.
Hii ni rekodi nyingine inawekwa na Yanga kwa mara ya pili baada ya ile ya kwanza ya mechi 49.
Misimu miwili iliyopita, Yanga ilivunja rekodi ya un-beaten mechi 37 iliyowahi kuwekwa na klabu za Azam Fc na Simba na Wananchi kuipeleka rekodi hiyo hadi mechi 49.
Kwa mara nyingine Wananchi wamevuka mechi 37 sasa wanaifukuzia rekodi yao wenyewe ya mechi 39.
Zimebaki mechi 12 kuhitimisha msimu huu, kama Yanga haitapoteza mchezo, itakwenda kuivunja rekodi yake ya mechi 49.
Mara ya mwisho Yanga kupoteza mchezo kwenye ligi ilikuwa Novemba 07 2024.
ADVERTISE HERE