Yawezekana hakuwa na mwanzo mzuri sana tangu alipojiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Vipers Fc, Mganda Allan Okello ameanza kudhihrisha ubora wake.
Jana katika ushindi wa mabao 3-0 ambao Yanga waliupata dhidi ya Pamba Jiji, Okello alihusika katika mabao yote matatu, akiwapa asisti Mudathir Yahya (x2) na Maxi Nzengeli.
Katika mechi iliyopita dhidi ya Tanzania Prisons, Okello alihusika katika mabao mawili akifunga moja na kutoa pasi ya bao la Mudathir ambaye unaweza kusema 'amewaka' sana msimu huu.
Katika mechi mbili Okello amehusika kwenye jumla ya mabao matano, akifunga moja na kutoa pasi nne za mabao.
Wale waliokuwa wakibeza usajili huu, ni muda sahihi kwao kumuomba radhi fundi huyu wa mpira, Star Boy...!


ADVERTISE HERE