Yanga imetinga robo fainali kombe la CRDB baada kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TMA Stars katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Bao pekee la Yanga katika mchezo huo lilifungwa na Maxi Nzengeli akimalizia pasi ya Edmund John.
Hata hivyo haikuwa mechi rahisi, maafande wa TMA Stars walikuwa na nidhabu kubwa kwenye ulinzi.
Iliwachukua Yanga dakika 69 kuifungua ngome ya TMA Stars na hatimaye kuibuka na ushindi uliowapeleka robo fainali.
Pengine Wananchi pia watajilaumu wenyewe kwa kutoibuka na ushindi mnono, eneo la umaliziaji limewaangusha.
Ushindi huo unaifanya Yanga iendeleze rekodi ya kibabe ya kutopoteza mchezo kwa takribani miaka 5 kwenye michuano hiyo.
ADVERTISE HERE