Yanga yarejea mazoezini kuiwinda Mbeya City

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Apr 2026
Yanga yarejea mazoezini kuiwinda Mbeya City

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TMA Stars juzi na kutinga robo fainali ya kombe la CRDB, kikosi cha Yanga leo kimerejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City.

Mchezo huo utapigwa Alhamisi, April 16 katika uwanja wa KMC Complex, saa 12:30 jioni.

Akizungumzia hali ya kikosi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema ni nyota wawili tu ambao wataendelea kuwa nje ukiwaondoa Dickson Job na Clement Mzize ambao wao hawatatumika mechi zilizosalia msimu huu.

Kamwe amesema winga Buba Jammeh alipata majeraha juzi kwenye mchezo dhidi ya TMA Stars, akiungana na Emmanuel Mwanengo ambaye anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja.

Kamwe amethibitisha kuwa mshambuliaji Prince Dube yuko fit kwa asilimia 100 na anaweza kutumika kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City huku Depu akiendelea kuimarika ambapo yeye ana asilimia 85 za kurejea mchezo unaofuata.

Aidha msemaji huyo wa mabingwa watetezi, amesema kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua ambaye alipata shida ya bega katika mchezo dhidi ya TMA Stars, anaendelea vizuri na atakuwa tayari kuikabili Mbeya City na mechi nyingine zinazofuata

Golikipa Djigui Diarra nae amerejea kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa mechi tatu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’