Zile mechi za viporo ambazo baadhi ya timu zilikuwa zikitambia sasa zimekwisha, mechi za mzunguuko wa 18 zimekamilika leo huku baadhi ya timu zikiwa tayari zimeanza kucheza mechi za mzunguuko wa 19.
Yanga imeendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 5 baada ya kukusanya alama 44 kutoka mechi 18.
Simba nayo imekamilisha mechi 18 iko nafasi ya pili ikiwa na alama 39, gap la pointi 5 sasa 'halina mbambamba'.
Azam Fc wanashika nafasi ya tatu wakikusanya alama 34 katika mechi 18 huku JKT Tanzania ikiwa ya nne na alama 29 baada ya mechi 18.
Unaweza kusema sasa safari ya Wananchi kuelekea ubingwa wa 5 mfululizo iko wazi kwani katika mechi 12 zilizobaki, watahitaji kushinda angalau mechi 10 na kuhakikisha hawapotezi dhidi ya Simba na Azam Fc.
