Goncalves afurahia rekodi ya kibabe ya mechi 30

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2026
Goncalves afurahia rekodi ya kibabe ya mechi 30

Kocha mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, ameweka rekodi ya kipekee baada ya kuiongoza klabu hiyo katika mechi 30 za mashindano yote, akipoteza mechi mbili pekee.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, Yanga imeshinda mechi 22, kutoka sare 6 na kupoteza 2, zote zikiwa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika mazingira magumu ya ugenini.

Akizungumza baada ya kufikia mafanikio hayo, Goncalves alisema rekodi hiyo ni matokeo ya juhudi za pamoja ndani ya klabu na si kazi ya mtu mmoja.

Amesema mafanikio hayo yanaonyesha uthabiti, nidhamu na mwendelezo mzuri wa kikosi chake tangu kuanza kwa msimu.

“Mechi 30, tukiwa tumepoteza mbili tu. Hii ni hatua muhimu sana katika safari yetu na Yanga. Inaonyesha uthabiti na mwendelezo wa kazi kubwa tunayofanya kila siku,” alisema Goncalves.

Kocha huyo aliongeza kuwa timu yake inaendelea kujenga msingi imara wenye malengo makubwa, ikiwa ni pamoja na kutawala mchezo kwa upande wa ushambuliaji na ulinzi.

“Tunaijenga klabu yenye kitu maalum: nafasi ya kwanza, mashambulizi bora na ulinzi bora. Hii ni kazi ya pamoja inayohitaji kujituma kila siku,” alisisitiza.

Katika kipindi hicho, Yanga imeonyesha kiwango bora ndani na nje ya nchi, huku ikionekana kuwa na muunganiko mzuri wa kikosi unaochangia matokeo chanya.

Hata hivyo, klabu hiyo imepata changamoto katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika, ambazo zimepotezwa ugenini dhidi ya AS FAR na Al Ahly.

Yanga imeendelea kuonyesha uimara kwenye mashindano ya ndani ikiongoza ligi kuu ya NBC ikiwa na alama 47 pia ikifanikiwa kutinga robo fainali ya kombe la CRDB.

Yanga haijapoteza mchezo kwenye ligi msimu huu ikiweka rekodi ya kucheza mechi 39 mfululizo bila kupoteza

Goncalves amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa sapoti yao kubwa katika kila mchezo, akisema mchango wao ni sehemu muhimu ya mafanikio ya timu.

“Ahsanteni sana mashabiki wetu. Kila uwanja mnasimama nasi. Sauti yenu ni nguvu yetu kubwa uwanjani,” alisema.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’