Jana klabu ya AS FAR ilifanikiwa kutinga fainali ya ligi ya mabingwa (CAFCL) ikiibuka na ushindi wa jumla wa mabao 2-1 dhidi ya RS Berkane.
AS FAR walishinda 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali mkondo wa kwanza na jana wakapoteza kwa bao 1-0.
AS FAR wamepoteza mechi mbili tu katika kampeni ya ligi ya mabingwa msimu huu. Mechi ya kwanza walifungwa na Yanga kwenye hatua ya makundi.
Timu hiyo ilikuwa kundi B sambamba na Yanga, Al Ahly na JS Kabylie. Walikata tiketi ya kutinga robo fainali kwenye mechi ya mwisho baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya Al Ahly wakati Yanga ikiishinda mabao 3-0 dhidi ya Kabylie.
Ni tofauti ya alama moja tu kati yake ya Yanga iliyowapa tiketi ya kutinga robo fainali ambao walivuka na sasa wako fainali.
Ni wazi kwa kile kilichoonekana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu, Yanga haiko mbali na kupata mafanikio makubwa katika michuano hiyo.