Pedro aandaa mkakati wa Kariakoo Derby bila Mudathir

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Apr 2026
Pedro aandaa mkakati wa Kariakoo Derby bila Mudathir

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves analazimika kukiandaa kikosi chake bila kiungo kiraka Mudathir Yahya kuelekea mchezo wa ligi kuu, dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba ambao utapigwa May 03 uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mudathir atakosa mchezo huo na mechi nyingine mbili zitakazofuata za ligi dhidi ya KMC na Coastal Union baada ya kufungiwa mechi tatu kutokana na tukio la kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa Mwanza.

Pedro amekiri kuwa atalazimika kufanya mabadiliko eneo analocheza Mudathir ambaye tayari alishatengeneza muunganiko na wachezaji wengine kwenye kikosi cha kwanza.

Amesema hakutarajia adhabu ya namna hiyo kwa kikosi chake kwasasa ambapo hata tukio husika hakuliona kwenye mechi hiyo mpaka alipokuja kuelezwa na wasaidizi wake.

"Nilishtuka sana niliposikia hiyo adhabu, kusema ukweli baada ya kufungiwa kwa Diara (Djigui) sikutegemea kama kutakuwa na kitu kama hicho, hata niliposikia hii ya Mudathir sikuliona hilo tukio mpaka wasaidizi wangu walipokuja kunikumbusha."

"Tuna timu nzuri na tuna viungo wazuri, tutaangalia ni nani anaweza kuja kuendelea pale ambapo tutamkosa Mudathir, tutatumia hizi mechi za Muungano kuweka mambo yetu sawa," alisema Pedro.

Pedro amesema Mudathir alikuwa ameanza kutengeneza muunganiko mzuri ambapo amepanga kuwakumbusha wachezaji wake wote kuwa makini na matukio ya kinidhamu ambayo yanaipunguzia nguvu timu yao.

"Sitaki kuwalaumu sana wachezaji wangu kutokana na wakati mwingine kuna matukio wanasababishiwa lakini kitu muhimu hapa nataka kuzungumza nao kuwakumbusha wanaichezea timu kubwa ambayo wakati mwingine timu zingine zinakuja kwa akili ya kuwaharibia.

"Wanatakiwa kuwa makini, kucheza kwa kutambua kwamba kuna watu wanawatafutia makosa, adhabu kama hizi zinaleta presha kwa timu, nafahamu tuna wachezaji wazuri ambao wanaweza kuziba nafasi ya Mudathir lakini kuna raha kuwa na wachezaji wako wote," aliongeza

Hata hivyo kifungo hicho hakimzuii Mudathir kushiriki michuano ya kombe la Muungano ambapo jana alikuwa sehemu ya kikosi kilichotinga nusu fainali baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Muembe Makumbi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
56m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’