Wakiwa Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Muungano, wachezaji wa Yanga, viongozi na benchi la ufundi jana wakapata nafasi ya kufanya utalii Zanzibar.
Kamisheni ya Utalii Zanzibar ndio iliyotoa mwaliko huo ambapo Wananchi walitembelea maeneo ya makumbusho Zanzibar.
Mabingwa hao wa kihistoria pia wakatembelea Kanisa la Anglican ambalo limebeba historia kwenye ukombozi wa haki za binadamu. Kanisa hilo lilijengwa eneo ambalo lilitumika kama soko la utumwa kabla ya 1873. Ujenzi wa kanisa hilo ulifanyika kuenzi Kukomeshwa kwa biashara ya utumwa visiwani Zanazibr.











ADVERTISE HERE