Bodi ya ligi (TPLB) imethibitisha mabadiliko ya uwanja wa mchezo namba 169 ligi kuu ya NBC kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopangwa kupigwa May 03.
Mchezo huo ambao awali ulipangwa kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, sasa utafanyika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa na Bodi ya ligi imebainisha kuwa mabadiliko hayo yametokana na uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa kwenye matengenezo.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 12 jioni.

ADVERTISE HERE