Ni rasmi sasa mchezo wa fainali kombe la Muungano ni kati ya Yanga dhidi ya Simba. Mchezo huo utapigwa Jumatano, April 29 katika uwanja wa New Amaan Complex.
Yanga na Simba zimefanikiwa kutinga fainali baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali.
Wananchi ambao ni mabingwa watetezi waliichapa Azam Fc mabao 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali huku watani zao Simba wakiichapa Mlandege mabao 3-0.
Baada ya fainali ya Muungano, May 03 wababe hao wa soka nchini wataumana kwenye mchezo wa ligi kuu uliopangwa kupigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
Mechi ya duru ya kwanza ligi kuu ilipigwa uwanja wa New Amaan Complex na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana, Jumatano ni mechi ya kukata mzizi wa fitma pale pale uwanja wa New Amaan Complex.
ADVERTISE HERE