Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ametua Zanzibar kushuhudia mchezo wa fainali kombe la Muungano kati ya Yanga dhidi ya Simba.
Mchezo huo utapigwa kesho Jumatano Aprili 29 saa mbili na robo usiku katika uwanja wa Amaan.
Hersi alikuwa Uswisi kwenye majukumu mengine kama Mwenyekiti wa umoja wa klabu barani Afrika (ACA).
Juzi alishuhudia mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam Fc akiwa nchini humo.

ADVERTISE HERE