Goncalves afunguka baada ya kupoteza Muungano Cup, kujipanga na mechi ya Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Apr 2026
Goncalves afunguka baada ya kupoteza Muungano Cup, kujipanga na mechi ya Jumapili

Baada ya kupoteza fainali ya Kombe la Muungano kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba SC, kocha mkuu wa Yanga SC, Pedro Gonçalves, ameibuka na ujumbe mzito wenye matumaini na mshikamano kwa mashabiki na timu yake.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, ulikuwa na ushindani mkubwa kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho. Dakika 90 za kawaida zilimalizika kwa sare ya bila kufungana, hali iliyosababisha kuongezwa kwa dakika 30 za muda wa nyongeza.

Ndani ya muda huo wa ziada ndipo Simba walipopata bao la ushindi kupitia mkwaju wa penati katika dakika za mwisho, na kuhitimisha mchezo huo wa dakika 120 kwa ushindi mwembamba wa 1-0.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Goncalves alionesha fahari kubwa kwa kikosi chake licha ya kupoteza taji hilo.

“Ninajivunia timu hii kwa namna tulivyopambana katika Kombe la Muungano. Tumeonesha kujitoa, tabia njema na umoja hadi dakika ya mwisho.”

Kocha huyo aliendelea kuwashukuru mashabiki wa Yanga maarufu kama Wananchi kwa sapoti yao isiyoyumba:

“Asanteni Wananchi kwa sapoti yenu ya ajabu, tunaihisi kila hatua ya safari yetu.”

Pamoja na matokeo hayo, Goncalves ameweka wazi kuwa macho yao sasa yapo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya watani zao hao ambao utpigwa May 03 uwanja wa Isamuhyo.

“Sasa tunahamishia nguvu zote kwenye mchezo wa Jumapili kwenye ligi tunayoiongoza nafasi ambayo tumeipata kwa juhudi zetu wenyewe na lazima tuendelee kuipigania.”

Aidha Goncalves amewataka mashabiki kuendelea kuwa bega kwa bega na timu yao.

“Tunahitaji muendelee kuwa nasi, sapoti yenu itakuwa muhimu. Tunaendelea kufanya kazi, tunaendelea kusukuma mbele — pamoja.”

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’