Kikosi cha Yanga bado kiko visiwani Zanzibar kikiendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Jumapili, May 1 katika uwanja wa Meja Jenerali, Isamuhyo.
Viingilio vya mchezo huo utakaopigwa saa 12 jioni vimewekwa hadharani ambao majukwaa ya Mzunguuko ni Tsh 15,000/-
Majukwaa mengine, VIP A ni Tsh 50,000/- na VIP B ni Tsh 30,000/-
Ikumbukwe uwanjaw a Isamuhyo unachukua takribani mashabiki 8,000 tu hivyo ni wazi ili kupata tiketi ni muhimu kukata mapema.
Mashabiki wa Yanga wameaswa kuchangamkia tiketi hizo mapema ili kuhakikisha wanakuwa kwa wingi siku ya Jumapili kuipa hamasa timu yao.
ADVERTISE HERE