Kiwango alichoonyesha mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi 'Jeshi' kwenye mchezo wa fainali kombe la Muungano dhidi ya Simba juzi, kimewakumbusha Wananchi umahiri wa beki huyo raia wa Ivory Coast.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza mkubwa wa kimashindano kwa Yao tangu aliporejea kutoka kwenye majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi nane.
Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves zaidi anamtumia Israh Mwenda kama chaguo lake la kwanza upande wa kulia lakini baada ya kazi aliyopiga Yao juzi, haitashangaza kama beki huyo atapewa nafasi nyingine ya kuanza kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Jumapili May 03 uwanja wa Isamuhyo.
Yao aliliweka salama eneo la upande wa kulia kwa muda wote ambao alikuwa uwanjani, hakukuwa na 'safari' upande wake.
Ni wazi alihitaji mechi moja tu ngumu ili kudhihirisha sasa amepona na yuko tayari kukabiliana na yeyote.



