Kuelekea mchezo mkubwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba SC na Yanga utakaopigwa Jumapili, Mei 03 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, hatua muhimu imepangwa kuchukuliwa ili kulinda uadilifu wa mchezo.
Imeelezwa kuwa wachezaji wote wa timu hizo mbili wanatarajiwa kufanyiwa vipimo vya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu (doping test) kabla ya pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki.
Hatua hiyo inakuja wakati kukiwa na mjadala mkubwa uliotawala mitandaoni ambapo baadhi ya mashabiki walihoji juu ya kinywaji chenye rangi ya zambarau kilichoonekana kikitumiwa na wachezaji wa Simba kabla na hata wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano.
Ingawa hakuna ushahidi rasmi uliothibitisha kuwepo kwa matumizi ya dawa zisizoruhusiwa, mjadala huo umeibua shauku ya kuona uwazi na haki vinatawala katika michezo hiyo mikubwa.
Hatua hiyo inalenga:
- Kulinda ushindani wa haki (fair play)
- Kuondoa sintofahamu kwa mashabiki
- Kuimarisha taswira ya ligi
Mchezo wa Jumapili una umuhimu mkubwa, Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwa msimu wa tano mfululizo