Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Machi 27 haujaisaidia Tanzania kuepuka maporomoko kwenye viwango vya soka vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa mwezi April.
Tanzania imeporomoka kwa nafasi tatu hadi ya 140 katika orodha ya Aprili Γ’β¬β Mei iliyotolewa jana na FIFA, huku Ujerumani ikiendelea kuongoza duniani, ikifuatiwa na Brazil, Ubelgiji, Ureno, Argentina, Uswisi, Ufaransa, Poland, Chle na Hispania zikikamilisha 10 Bora.
Kwa Afrika, Tunisia ndiyo inaongoza ikiwa nafasi ya 21 duniani, ikifuatiwa na Senegal 27, DRC 38, Morocco 41, Misri 45, Ghana 47, Nigeria 48, Cameroon 49, Mali 64 na Cape Verde 65 ikikamiklisha 10 Bora za Afrika.
Tanzania inazidiwa na jirani zake wote wa Afrika Mashariki, Uganda ikikamata nafasi ya 82 na Kenya nafasi ya 112.

ADVERTISE HERE