Goncalves awapongeza wachezaji Yanga kwa 'ushujaa'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 May 2026
Goncalves awapongeza wachezaji Yanga kwa 'ushujaa'

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amewapongeza wachezaji wake kwa ushujaa na moyo wa upambanaji walionyesha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba jana ambapo walilazimika kutokea nyuma kwa mabao 2-0 na kulazimisha sare ya 2-2.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Goncalves alisema hawakuwa na wakati mzuri kwenye dakika 15 za kwanza wakijikuta wanaruhusu mabao mawili ya haraka.

Hata hivyo Goncalves alisema baada ya vijana wake kurejesha utulivu, walikuwa bora zaidi na pengine walistahili kushinda mchezo huo.

"Hatukuwa vizuri kwenye dakika 15 za kwanza lakini tukizungumzia dakika 75 au 80 zilizofuata nafikiri tulicheza vizuri sana"

"Tulianza vizuri lakini tukafanya makosa, hatuwezi kupoteza umakini katika nyakati kama zile, tunazungumza sana kuhusu mambo haya."

"Makosa kama yake yanampa mpinzani wako faida na kupunguza kujiamini kwa timu kwa ujumla"

"Nawapongeza wachezaji wangu licha ya changamoto hiyo waliendelea kupambana na kufanikiwa kurejea mchezoni. Nafikiri kwa ujumla tulikuwa timu bora zaidi ya Simba."

"Tulistahili kushinda lakini tuna alama tano mbele ya wapinzani wetu wakuu katika mbio za ubingwa. Tutaendelea kupambana katika mechi 10 zilizobaki ili tuweze kutetea ubingwa wetu."

Goncalves alizungumzia uamuzi wake wa kumuanzisha Israel Mwenda upande wa kulia kabla ya kumtoa wakati wa mapumziko nafasi yake ikichukuliwa na Yao Kouassi.

"Wakati mwingine tunahitaji kuzingatia mbinu za mchezo na aina ya wachezaji tunaohitaji kuwatumia. Lengo ni kuhakikisha tunawatumia wachezaji sahihi na kuwapunguzia mzigo wachezaji wengine, ni bahati mbaya jambo hili baadhi hawaelewi," aliongeza Goncalves.

Baada ya kuingia Yao alionekana kuimarisha zaidi safu ya ulinzi upande wa kulia kama alivyofanya kwenye mchezo wa fainali kombe la Muungano April 29 visiwani Zanzibar.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’