Yanga yaanza mapema kusaka kiungo mkabaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2026
Yanga yaanza mapema kusaka kiungo mkabaji

Klabu ya Yanga imeanza mapema mipango ya kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao, ikiwa ni pamoja na kusaka kiungo mkabaji mpya atakayeimarisha eneo la kiungo wa ulinzi.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, uongozi wa Yanga umeanza mchakato wa ufuatiliaji wa wachezaji kadhaa wa kimataifa, huku jina la kiungo wa Klabu ya Zoman FC, Mamadou Thierno, likitajwa kuwa miongoni mwa wanaofuatiliwa kwa karibu zaidi.

Kwa sasa, eneo la kiungo mkabaji ndani ya Yanga linategemewa zaidi na wachezaji kama Mohamed Damaro pamoja na Duke Abuya, ambao wamekuwa wakipishana katika nafasi hiyo kutokana na mahitaji ya kikosi.

Kumekuwa na maoni tofauti kuhusu aina ya uchezaji wa Damaro ambaye imekuwa nadra kwake kumaliza dakika 90 bila kupewa jambo ambalo wachambuzi wa soka wanaona hawezi kuwa mchezaji wa kutegemewa katika nafasi hiyo.

Damaro alitua Yanga kwa mkopo kwenye usajili wa dirisha dogo Januari 2026 akitokea klabu ya Singida BS. Habari njema ni kuwa Damaro ni mchezaji wa ndani hivyo Yanga inasaka mchezaji wa kigeni ambaye atachukua nafasi ya Moussa Balla Conte aliyetolewa kwa mkopo klabu ya Raja CA.

Thierno aonekana kuwa chaguo sahihi

Mamadou Thierno anacheza kama kiungo namba 6 (defensive midfielder), nafasi ambayo inahitaji nguvu, akili ya mchezo na uwezo wa kusoma hatari mapema.

Mafanikio yake hadi sasa yanaonesha ubora wake kama mchezaji wa kiwango cha juu:

  • Msimu uliopita alitwaa tuzo ya kiungo bora wa ulinzi
  • Msimu huu ametajwa kwenye kikosi bora cha wiki mara 7 kwenye ligi ya Ivory Coast
  • Msimu huu tayari amefunga mabao 2 na kutoa asisti 2

Takwimu hizo zimeifanya Yanga kuona uwezekano wa kupata kiungo atakayesaidia kuongeza ubora na kina katika kikosi chao, hasa katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Mkakati wa mapema sokoni

Vyanzo vya karibu na klabu vinaeleza kuwa Yanga imeamua kufanya kazi mapema sokoni ili kuepuka ushindani mkali wa usajili unaojitokeza mwishoni mwa msimu. Lengo kuu ni kuhakikisha kikosi kinaendelea kuwa imara na chenye ushindani katika kila idara.

Iwapo mazungumzo yatafanikiwa, Mamadou Thierno anaweza kuwa miongoni mwa nyota wapya wa kuimarisha kikosi cha YangaΒ kuelekea msimu ujao.

Pamoja nae, Yanga pia inaelezwa ilifanya mazungumzo na kiungo wa Azam Fc James Akamiko ambaye mkataba wake na Azam Fc unamalizika mwshoni mwa msimu. Hata hivyo inaelezwa kiungo huyo bado hajafanya maamuzi juu ya hatma yake.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’