Mechi ya Ligi Kuu NBC kati ya Simba na Yanga iliyochezwa katika Uwanja wa Meja Jenerali na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, imeendelea kuzua mjadala kufuatia tukio tata la dakika za mwisho lililohusisha madai ya penati.
Katika tukio hilo lililotokea katika eneo la hatari, mshambuliaji wa Yanga Laurindo Aurelio (Depú) alionekana kuangushwa baada ya kuguswa na kiwiko cha beki wa Simba, Ismail Toure, ndani ya eneo la hatari dakika za lala salama.
Hata hivyo, mwamuzi wa kati kutoka Morocco Hamza El Faruq aliyesimamia mchezo huo aliamua kuendelea na mchezo bila kutoa penalti wala adhabu ya kadi.
Ni wazi tukio hilo lilikuwa na dalili za wazi za kosa ndani ya eneo la hatari, Toure alikuwa katika nafasi ya mwisho ya ulinzi na hivyo angeweza hata kupewa kadi nyekundu pamoja na penalti kwa Yanga.
Hapa Yanga walinyimwa nafasi muhimu ya kupata ushindi katika mchezo huo kutokana na uamuzi huo wa utata, ambao umefungua upya mjadala kuhusu ulazima wa mechi za Derby ya Kariakoo kuchezeshwa na waamuzi kutoka nje ya nchi.
Kwa ujumla, waamuzi wa mchezo huo wote walitoka na Morocco na kulikuwa na maamuzi mengi ambayo wengi wanaona hayakuwa fair.