Kikosi cha Yanga leo kinarejea mazoezini kukamilisha maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC utakaopigwa kesho Jumatano, May 06 katika uwanja wa KMC Complex.
Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema alitoa siku moja ya mapumziko kwa wachezaji wake baada ya mchezo dhidi ya Simba.
Amesema leo wanarejea kambini wakiwa na nguvu mpya lengo lao likuwa kuibuka na ushindi dhidi ya KMC.
"Baada ya mchezo dhidi ya Simba tulitoa mapumziko ya siku moja. Tumekuwa na mfululizo wa mechi hivyo ilikuwa muhimu kuwapa wachezaji mapumziko ili kujipanga upya."
"Tunatambua ugumu wa mchezo dhidi ya KMC, wako katika jitihada za kujinusu na kuteremka daraja hivyo hatupaswi kuwadharau."
"Tunapaswa kujiandaa vyema kuelekea mchezo huo pamoja na ratiba ya mechi mfululizo zitakazofuata," alisema Pedro.
Baada ya kumalizana na KMC, Yanga itarudi tena dimba la KMC Complex baada ya siku tatu kuikabili Coastal Union.