Yanga imeondoka na alama tatu muhimu uwanja wa KMC Complex baada ya kuichapa KMC bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
'Star Boy' Allan Okello alifunga bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo kwenye kipindi cha pili akipiga shuti la chini nje kidogo ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Shekhan Khamis.
Yanga mchezo huo kwa kasi kwenye kipindi cha kwanza lakini kukosekana kwa umakini eneo la mwisho ilipelekea Yanga kupoteza nafasi nyingi.
Kadiri mchezo ulivyokuwa ukiendelea ndivyo KMC walivyoongeza kujiamini wakiweka ulinzi mkali kwenye eneo lao.
Hata maajabu ya Okello aliyeng'ara kwenye mchezo huo, yaliihakikisha Yanga kuondoka na alama tatu ambazo zinawafanya wazidi kujichimbia kileleni baada ya kufikisha alama 51.



ADVERTISE HERE