Mshambuliaji Clement Mzize ameanza kufanya mazoezi mepesi ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa miezi kadhaa sasa.
Mzize ameanza program ya maalum chini ya uangalizi wa daktari baada ya kukamilika kwa hatua ya uponaji wa jeraha baada ya upasuaji aliofanyiwa Afrika Kusini mwezi Februari.
Hatua hiyo ni muhimu ili kuhakikisha taratibu zote za uponaji wake zinakamilika kabla ya kuanza rasmi mazoezi ya timu.
Kwa muda uliobaki kuhitimisha msimu huu, ni wazi atautumia kujiimarisha na pengine ataungana na wachezaji wengine kwenye mazoezi ya pre-season kuelekea msimu ujao.
Naye beki Dickson Job ameanza kufanya mazoezi mepesi ya Gym ikiwa ni sehemu ya program za kumsaidia kupona vyema.

Job aliumia kwenye mchezo dhidi ya Simba March 1 nae kwa mujibu wa taarifa ya Yanga, atarejea kikosini wakati wa pre-season kuelekea msimu ujao