Kama vipi sawa, tuwaachie Kagame Cup yao

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
8 Jun 2018
Kama vipi sawa, tuwaachie Kagame Cup yao
Moja ya sababu iliyopelekea Yanga na Simba kupangwa katika kundi moja kwenye michuano ya CECAFA Kagame Cup ni suala la mapato.

Waandaaji wa michuani hiyo wanaamini mpambano utakao zikutanisha timu hizo ndio utakaotengeneza 'mkwaja nrefu'.

Hapa Yanga itakuwa inatumiwa na waandaaji kwa ajili ya maslahi tu.

Lakini ukweli unabaki palepale kuwa msimu huu Yanga imeshiriki michuano ya Kimataifa kama 'mtoto yatima'.

TFF ilitoa msaada mdogo sana kwa mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania Bara.

Leo hii Yanga ikiamua kujitoa kwenye michuano ya Kagame ili kujipa muda wa kufanya maandalizi ya michuano ya kombe la Shirikisho, haitakuwa inakosea.

Msimu uliomalizika Yanga ilikumbana na ratiba ya 'ajabu' iliyokuwa na mpangilio wa hovyo ambayo kwa kiasi kikubwa ulichangia Yanga kufanya vibaya katika michezo ya mwishoni mwa msimu.

Ni hii hii TFF ambayo leo inataka Yanga ishiriki michuano ya kombe la Kagame ili itengeneze pesa, haikuona umuhimu wa kuisaidia Yanga wakati ligi ikiendelea kwa kuikomoa na kuipangia ratiba icheze kila baada ya siku mbili.

Nakumbuka kabla ya Simba kwenda Misri kucheza na Al Masry ilipewa mapumziko ya karibu wiki mbili ili iweze kujiandaa lakini hali haikuwa hivyo kwa Yanga.

Kuna wakati Yanga ilikwenda kucheza Shelisheli na St Luis, siku mbili baadae ikacheza na Majimaji kombe la FA mkoani Ruvuma, siku mbili tena ikacheza na Ndanda FC mkoani Mtwara kwenye mchezo wa ligi.

Baada ya wadau kulalamika, mchezo uliokuwa unafuata siku mbili baadae dhidi ya Mtibwa Sugar ndio ukaahirishwa na hapo Yanga ikapata ahueni kujiandaa na mchezo wa nyumbani dhidi ya Township Rollers.

Ratiba hiyo ilijirudia tena kwenye michezo ya mwisho ya kumaliza msimu mpaka kupelekea uongozi wa Yanga kuamua kugawa vikosi viwili, kimoja kikibaki Dar kujiandaa na mchezo dhidi ya Rayon Sports, kingine kikienda mikoani kukamilisha ratiba.

Kwenye michuano ya kombe la FA Yanga ndiyo timu pekee ambayo ilicheza michezo yake yote ugenini!

Sasa kwa kuwa michuano hii ya Kagame sio ya lazima, haitakuwa vibaya kama Yanga itajitoa ili kujiandaa na michuano muhimu ya kombe la Shirikisho.

Uamuzi huu ukifikiwa utawagutusha TFF kuona umuhimu wa kulinda maslahi ya timu zake zinazoshiriki michuano mingine kuliko kulinda maslahi ya baadhi ya timu pekee.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’