Mikiki mikiki ya Ligi Kuu ya Wanawaken (WPL) inaendelea leo ambapo mechi kubwa inayokutanisha watani wa jadi Simba Queens na Yanga Princess itapigwa uwanja wa Azam Complex.
Mechi hii imeshikilia rehani ya mbio za ubingwa kwa Yanga Princess wakihitaji kushinda.
Yanga Princess iko nyuma ya Simba Queens kwa tofauti ya alama nne, ushindi leo utapunguza gap kusalia alama moja.
Matokeo tofauti na ushindi kwa Yanga Princess yatafifisha matumaini ya kinadada hao Wananchi kutwaa ubingwa msimu huu.
Msimu huu Yanga Princess imeonyesha uimara ikipoteza mechi mbili tu moja ikiwa dhidi ya Simba Queens mchezo wa duru ya kwanza.
Leo Wananchi wanahitaji matokeo ya aina moja tu, USHINDI ili kubaki katika mbio za ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake.
ADVERTISE HERE