Kocha wa Yanga Abdihamid Moalin amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa robo fainali kombe l CRDB dhidi ya JKT Tanzania.
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, May 16 katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es salaam.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Moalin amesema wanafurahi kucheza katika hatua hiyo na wamepania kusonga mbele nusu fainali.
"Sisi tumejiandaa vyema, tuko tayari kwa mchezo huu wa robo fainali. Tunafurahi kucheza katika hatua hizi kwani tumezoea."
"Tunatambua hautakuwa mchezo mwepesi kwa sababu tunakutana na timu nzuri lakini tumejiandaa kushinda," alisema Moalin.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 12:30 jioni ambapo mshindi atasonga mbele hatua ya nusu fainali.
Kama dakika 90 zitahitimishwa bila mshindi, changamoto ya mikwaju ya penati itatumika kupata timu ya kutinga nusu fainali