Jana katika mchezo wa robo fainali kombe la CRDB dhidi ya JKT Tanzania, kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua aliwakumbusha maafande hao yeye ni nani.
Katika mchezo ambao kocha wa JKT Tanzania Ahmed Ali ni kama aliweka mkakati kwenye safu yake ya ulinzi kumdhibiti Pacome, mambo yalikuwa tofauti, Pacome akiondoka na tuzo ya nyota wa mchezo.
Mabao yote yaliyofungwa na Yanga kwenye mchezo huo yalipita mguuni kwa Pacome. Pasi yake kwa Chadrack Boka ilizaa bao la kwanza la kujifunga beki wa JKT Tanzania huku Mudathir Yahya akiongeza bao la pili kutokana na pasi mpenyezo ya nyota huyo raia wa Ivory Coast.
Kulikuwa na 'battle' ya aina yake kati ya Pacome na walinzi wa pembeni wa JKT Tanzania ambao waliishia kumfanyia madhambi na kuzawadiwa kadi za njano.

