Msimu huu Yanga na Azam Fc tayari zimekutana mara mbili katika mechi ya ligi kuu na kombe la Muungano.
Mchezo wa ligi kuu ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana huku Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Muungano.
Bado kuna dakika nyingine 180 za Derby ya Dar es salaam, baada ya timu hizo kutinga nusu fainali ya kombe la CRDB.
Yanga na Azam Fc zitamenyana kwenye mchezo wa nusu fainali kusaka tiketi ya kukutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba dhidi ya Coastal Union kwenye fainali.
Ikumbukwe pia timu hizo bado hazijamalizana mechi ya duru ya pili ligi kuu ya NBC, Yanga wakitarajiwa kuwa wenyeji wa mchezo huo.
Kocha Abdihamid Moalin na benchi lake la ufundi wana kazi ya kufanya kuhakikisha Yanga inaibuka kidedea katika mechi hizo mbili ili kuwa na nafasi ya kutetea mataji yake yote mawili.
Mechi zote mbili zinatarajiwa kupigwa mwezi Juni 2026.