Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa robo fainali kombe la CRDB, Kocha Mkuu wa Yanga Abduhamid Moalin aliwapa wachezaji mapumziko ya siku mbili.
Leo Yanga inarejea kambini kukamilisha maandalizi ya mchezo unaofuata wa ligi kuu dhidi ya Singida BS ambao utapigwa Ijumaa, May 22 uwanja wa KMC Complex.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa wamoja na kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenye kila mchezo ili kuwaunga mkono wachezaji wao.
Kamwe amesema kila mechi iliyobaki ni kama fainali kwani hakuna tena nafasi ya kufanya makosa.
"Niwaombe mashabiki wa wanachama tuwe pamoja katika kipindi hiki, tuna mechi 9 za kutetea mataji yetu mawili."
"Tuiunge mkono timu yetu kwa kujitokeza viwanjani kwa wingi, wakati huu hatuhitaji mashabiki wachambuzi wa mitandaoni tu," alisema Kamwe.
Tayari wapinzani wao Singida BS wako jijini Dar es salaam wakitokea mkoani Tanga ambako walitupwa nje ya michuano ya kombe la Shirikisho la CRDB kwa kipigo dhidi ya Coastal Union